Mungu, Baba yetu mwenye upendo, tunakusifu na
kukushukuru kwa zawadi ya miaka ishirini na tano
(25) ya Jimbo letu la Maralal.

                                                                                                        
Kwa mioyo ya shukrani, tunakushukuru kwa neema
imani, tumaini, upendo na baraka ulizotujalia
tunapoadhimisha mwaka huu wa Jubilei.
Utufanye kuwa watu wanaotembea pamoja katika
tumaini.
Uwabariki Maaskofu, mapadre, masista
waseminaristi na makatekista wetu. Tunaomba pia
kwa ajili ya zawadi ya miito zaidi katika Jimbo letu.
Uwaimarishe wazazi katika wito wao, uponye mioyo
iliyojeruhiwa na mahusiano yaliyovunjika.
Uwaongoze watoto na vijana wetu, na uzifanye

parokia zetu ziwe mahali ambapo upendo wako
unashuhudiwa.
Uzifanye upya huduma zetu za kichungaji kwa Roho
wako Mtakatifu, ili familia zetu ziwe makanisa iliyo
hai na kweli, zilizojengwa juu ya sala, msamaha
amani na upatanisho, tunapoishi Injili kwa furaha.
Mimina Roho wako Mtakatifu juu ya Jimbo letu, ili
tukitembea pamoja katika imani, tutumikie kwa
unyenyekevu na furaha, na tuendelee kwa uaminifu
utume wa Kristo sasa na kwa vizazi vijavyo.
Watakatifu Petro na Paulo

Mtuombee. Amina
2001-2026

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *